Bei ya pikipiki iliyotumika au Used Tanzania inatofautiana kulingana na brand, mtindo, mwaka wa utengenezaji, na hali ya pikipiki. Kwa ujumla, pikipiki zilizotumika za chapa au Brand za Kichina kama vile Toyo, Boxer, na nyingine zinapatikana kwa bei nafuu zaidi kuliko pikipiki za brand za kimataifa kama vile Honda, Yamaha, na Suzuki.
Bei ya pikipiki iliyotumika ya Brand za Kichina kama vile Toyo au Boxer yenye ujazo wa cc 125 inaweza kuanzia shilingi milioni 1.5 hadi milioni 3. Bei ya pikipiki iliyotumika ya chapa za kimataifa kama vile Honda au Yamaha yenye ujazo wa cc 125 inaweza kuanzia shilingi milioni 3 hadi milioni 5 au zaidi kulingana na hali ya pikipiki.